Bajeti kilimo yaongezeka kwa asilimia 29

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewasilisha bajeti ya 2023/2024, ya  Shilingi 970.78  bilioni katika mafungu matatu ikiwa imeongezeka kwa asilimia 29.24 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2022/2023 ya Sh.751.12 bilioni.

Akiwasilisha bajeti hiyo leo Jumatatu Mei 08, 2023, Waziri Bashe  amesema kati ya Sh 577.71 bilioni zinaombwa kati ya fedha hizo, Sh 465.69 bilioni  ni kwa ajili ya kutekeleza  miradi ya maendeleo ambapo Sh 365.64 bilioni  ni fedha za ndani na Sh 100.05 bilioni ni fedha za nje.

Amesema, Sh 112.01 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Sh 56.55 bilioni  ni kwa ajili ya mishahara ya Wizara ,Sh115.55 bilioni  ni kwa ajili ya matumizi mengineyo ya Wizara,Bodi na Taasisi.

Waziri  Bashe  amesema kati ya Sh 373.51 bilioni za Tume ya Umwagiliaji, Sh 299.96 bilioni ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na  Sh73.54 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Amesema kati ya fedha za maendeleo zinazoombwa, Sh 288.464 ni fedha za ndani na Sh 11.5 bilioni  ni fedha za nje.

Waziri Bashe amesema Sh73.54bilioni  ya fedha za Matumizi ya Kawaida zinazoombwa kati ya fedha hizo Sh 66.33 bilioni  ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo  na Sh 7.21 bilioni  ni kwa ajili ya Mishahara.

Bashe ambaye pia ni mbunge wa Nzega (CCM) amesema  Sh.17 bilioni  zinazoombwa kwa ajili ya  kutekeleza miradi ya maendeleo kati ya fedha hizo  zinazoombwa, Sh  1 bilioni ni fedha za ndani na Sh 1.17 bilioni ni fedha za nje.

Habari Zifananazo

Back to top button