Bajeti kufadhili magari ya rais, mkewe Nigeria

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu ametia saini na kuwa sheria bajeti ya ziada ya Dola bilioni 2.8 ambayo inajumuisha ufadhili wa magari mapya ya kuzuia risasi kwa ajili yake na mkewe, licha ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya raia. Mtandao wa Reuters umeripoti.

Taarifa ya mtandao huo imeeleza kuwa bajeti hiyo iliidhinishwa na wabunge Novemba 2, pia inajumuisha mgao wa boti ya rais, magari rasmi kwa ajili ya ofisi ya mke wa rais, na ukarabati wa makao ya rais.

Mpango wa matumizi ya fedha hapo awali ulipendekezwa na Tinubu kama njia ya kushughulikia maswala ya dharura kama vile ulinzi na usalama.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button