Bajeti ya Kenya sh trilioni 63.2

SERIKALI ya Rais William Ruto imewasilisha bajeti yake ya kwanza ya Sh trilioni 3.7 za kenya (TSh trilioni 63.2) ikipania kulipa madeni yote ikiwa ni pamoja na deni la taifa ambalo limefikia asilimia 67 ya Pato la Taifa.

Waziri wa Fedha wa Kenya, Njuguna Ndung’u amesema Alhamis kuwa “Pamoja na kwamba mzigo wa deni umeongezeka…Serikali imejizatiti kutekeleza majukumu yote ya kulipa deni la umma kadri inavyowezekana.

“Tumedhibiti matumizi yetu ili kuhakikisha thamani ya pesa,” alisema waziri.

Upinzani umekataa msururu wa nyongeza ya ushuru uliopendekezwa na serikali ya Rais William Ruto, ambao ni muhimu ili kuleta utulivu wa fedha za serikali katika kukabiliana na kuongezeka kwa ulipaji wa madeni.

Habari Zifananazo

Back to top button