BAKWATA Dar yakabidhi Vifaa vya huduma za kijamii Muhimbili, Ocean Road

DAR ES SAALAM: BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Dar es Salam wametoa misaada kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Akizungumza leo wakati wakati wakitoa misaada hiyo kaimu Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam,Walid Omary amesema wameshiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo usafi SoKo la Samaki Feri ikiwa ni kuendana na kaulimbiu ya Wiki ya Maulid ya “mtume na jamii”.
Amesema Kama viongozi mpango wao ni kuendelea kuhamasisha usawa kwenye jamii Kwa maslahi ya Taifa bila kujali Dini wala kabila la mtu dhamira ni moja tu kutoa misaada Kwa wenye uhitaji.
“Niwaombe watanzania na jamii Kwa Ujumla kuona umuhimu wa kujijengea utamaduni wa kutembelea ndugu zetu wenye matatizo waliopo hospitalini na kuwafariji sio lazima kusubiri hadi augue ndugu yako ndio utembelee maeneo hayo tukumbuke kuugua pia ni sehemu ya ibada.
Mwenyekiti wa BAKWATA Mkoa huo Sheikh. Dk Hussein Afif amesisitiza umuhimu wa jamii kuungana kusaidia wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa walio katika hospitali mbalimbali kuwawezesha nao kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.