Bakwata: Tuna imani kubwa na serikali

DODOMA: BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limesema linamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yote na kuwaombea dua ili waweze kuwa na ufanisi zaidi.

Akisoma salamu za Bakwata katika Baraza la Maulid Kitaifa mkoani Dodoma leo Septemba 28, 2023, Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaj Nuhu Mruma amesema, sababu za wao kuiunga mkono serikali ni kutokana na juhudi inazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Serikali imekuwa ikiwaletea wananchi maendeleo kwenye sekta za kiuchumi, kisiasa na kijamii pamoja na kuboresha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hatuna budi kuiunga mkono,”amesema.

Amesema katika kujenga demokrasia nchini, Rais Samia Suluhu Hassan aliunda kikosi kazi maalum kilichoshughulikia masuala ya demokrasia na hatimaye kuyakubali maoni mengi yaliyopendekezwa na kikosi kazi hicho.

“Na mengine yameanza kufanyiwa kazi ikiwemo ruhusa ya vyama vya siasa kufanya mikutano yao ya hadhara, tunampongeza sana Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan,” amesema Mruma.

Amesema jukumu lao viongozi wa dini ni kuendelea kuishauri serikali, kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mambo mbalimbali na kuiombea amani nchi pamoja na kuwaombea viongozi wake.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button