Bakwata yatakiwa kujenga vyuo vya ufundi
Mufti akemea fitna, majungu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, ametoa ushauri kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kufikiria kujenga shule za ufundi zitakazowawezesha vijana kupata ujuzi wa kuwaingiza kipato.
Kinana ametoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Ushauri huo wa Kinana unatokana na maelezo aliyopewa kuhusu majengo yatakayojengwa katika eneo hilo ni pamoja na shule ya msingi na sekondari.
Mnampango wa kujenga shule ya sekondari, shule za msingi, kwa ushauri wangu jengeni shule za ufundi, shule za sekondari ni nyingi, shule za serikali ni nyingi, mkijenga shule mtataka watu walipie wakati serikali inatoa elimu bure.
“Tunao mfano wa shule za Jumuiya za Wazazi zinapata tabu kwa sababu wanaokwenda kusoma wanatakiwa kulipa, lakini mwanafunzi akijua kuna shule ya ufundi inayofundisha uwashi, ufundi umeme, udereva, ufundi magari, yuko tayari kusoma kwa sababu anajua atapa kazi.
“Shule ambazo tunasoma nyingi zaidi ya cheti hakuna tunachopata, ni bora ukawa na cheti cha ufundi kuliko kumaliza kidato cha sita.
Ukiwa fundi hata usipoajiriwa unaweza kujiajiri na mtu ukapata riziki yako ya kila siku,” alisema Kinana.
Kutokana hali hiyo, Kinana aliihimiza BAKWATA kujenga vyuo vya ufundi ili wananchi wapate taaluma ya mikono yao,” amesema.