Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Wales na klabu ya Real Madrid, Gareth Bale ametangaza kushiriki katika hafla ya mashindano ya ‘PGA Tour’ ya mchezo wa gofu ikiwa ni wiki chache baada ya kutangaza kustaafu soka.
Bale alisema atashiriki katika mashindano ya AT&T Pebble Beach Pro-Am yatakayofanyika Februari huko California nchini Marekani.
Nyota huyo wa zamani wa Tottenham mwenye umri wa miaka 33 alistaafu mapema mwezi huu baada ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi Wales na mfungaji bora wa mabao wa timu ya taifa.
“Nafurahi kutangaza nitacheza katika AT&T Pebble Beach Pro-Am mwanzoni mwa mwezi ujao, twende pamoja.” alisema Bale.