Baleke apiga ‘hat-trick ya kwanza

STRAIKA wa Simba SC, Jean Baleke amefunga ‘Hat-trick’ yake ya kwanza katika mchezo wa ligi kuu ulioisha kwa timu hiyo kushinda mabao 3-0 katika Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Baleke amefunga mabao hayo dakika ya 3, 7 na 34 ya kipindi cha kwanza. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 57 ikiwa nafasi ya pili, huku ikiwa imecheza michezo 24 nyuma ya Yanga wenye michezo 24.

Wapinzani wao Mtibwa Sugar wanabaki kwenye nafasi yao ya tisa wakiwa na pointi 29, ikiwa imecheza michezo 25.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Habari Zifananazo

Back to top button