Baleke ni mali halali Simba

SIMBA SC imesema mshambuliaji wao, Jean Baleke ni mchezaji  halali kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini, Ahmed Ally amesema TP Mazembe walipewa pesa yao na ametumikia kandarasi yake miezi minne akiwa Simba SC.

“Niwatoe shaka wana Simba ya kwamba Baleke bado yupo sana Simba kwa muda mwingine, mpaka sasa hakuna ofa yoyote kutoka klabu yoyote ikimuulzia Baleke,”amesema Ahmed.

Akifafanua kuhusu tetesi za kuondoka kwa wachezaji wengine, Ahmed amesema kipa Aishi Manula bado ana mkataba wa miaka miwili na Simba, hivyo ataendelea kuitumikia klabu yake.

Kwa upande wa beki, Mohammed Hussein, Ahmed Ally amesema: “hana popote pa kwenda duniani zaidi ya Simba.”

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button