Balozi Mbega: Serengeti Girls imetoka kishujaa

Serengeti Girls imeweka historia kwa kutinga hatua ya robo fainali

BALOZI wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega amesema licha ya Serengeti Girls kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17, wawakilishi hao hawatakiwi kujisikia ‘wanyonge’.

Akizungumza wakati alipoitembelea timu hiyo hotelini baada ya timu kutolewa na Colombia kwa mabao 3-0 katika mechi ya hatua ya robo fainali nchini India, mwanadiplomasia huyo hatua waliyofika ni kubwa.

“Hapo tulikuwa tukiwafariji ili wachangamke wasijisikie wanyonge. Na waone kuwa hatua waliyofikia ni kubwa mno kwao wao na nchi kwa ujumla,” amesema.

Balozi aliitembelea timu hiyo kuwaaga mashujaa hao ambao wameliwakilisha taifa vema katika mashindano hayo ya kimataifa.

“Baada ya kumalizika mechi nilikwenda kuwaaga na kula nao chakula kabla hawajaondoka,” ameieleza HabariLeo na SpotiLeo.

Awali, kabla ya kukabiliana na Colombia, Rais Samia Suluhu Hassan aliwatakia wachezaji hao kila la heri katika mchezo wa robo fainali kwa kuandika:

 

Habari Zifananazo

Back to top button