Balozi wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega ameisifu timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 licha ya kupoteza mechi dhidi ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Japan.
Wawakilishi hao wa Tanzania walikubali kipigo kizito cha 4-0 nchini India yanapofanyika mashindano hayo ya dunia.
“Sisi tuliokuwa pale uwanjani tulishuhudia, hawa vijana wamejitahidi sana, lakini nimezungumza na Kocha, amenihakikishia watajipanga ili waweze kufanya vizuri zaidi,” HabariLeo Online imemnukuu Balozi.
Hata hivyo, amemmiminia sifa kipa wa Serengeti Girls kwa ushupavu aliouonesha kwa kuzuia michomo kutoka kwa washambuliaji wa Japan.
Akielezea Japan, Mwanadiplomasia huyo amesema timu hiyo ina wachezaji waliojengeka hivyo kitendo cha kuruhusu magoli hayo huku India ikiwa na historia ya kuchabangwa 8-0. Kufungwa magolo manne Tanzania imejitahidi.
Sauti ya Balozi Anisa Mbega kuhusu matokeo ya Serengeti Girls dhidi ya Japan na wito wake kwa Watanzania kuelekea mechi zijazo
Ametoa wito kwa Watanzania kuungana na kuiombea timu hiyo ili iweze kufanya vema katika mechi zilizobaki.
Mbali na Japan, wapinzani wengine wa Tanzania katika kundi D ni Ufaransa na Canada.
Kabla ya pambano hilo la la jana dhidi ya Japan, Balozi Mbega aliitembelea kambi ya Serengeti Girls kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji.
Comments are closed.