Balozi wa Rwanda ashiriki usafi Arusha

BALOZI wa Rwanda nchini Tanzania, Meja Jenerali, Charles Karamba, amewataka wananchi wa Jiji la Arusha kujenga tabia ya kufanya usafi wa mazingira yao mara kwa mara, ili kuvutia watalii na kuweka taswira nzuri ya nchi kimataifa.

Akizungumza leo jiijini Arusha, wakati aliposhiriki shughuli ya usafi, katika eneo la soko kuu na stendi kuu ya mabasi, Meja Jenerali Karamba,  alisema usafi huweka taswira ya nchi vizuri duniani na kuvutia wengi.

“Jengeni tabia ya kufanya usafi mara kwa mara, ukiangalia Arusha ni kitovu cha utalii, hii itasaidia kuweka taswira nzuri ya nchi kimataifa na usafi huepusha¬† uzalishaji wa wadudu wanaoleta magonjwa ya mlipuko,” alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Saidi Mtanda ameshukuru  balozi huyo na watu wengine kutoka Rwanda kushiriki katika shughuli ya usafi, ambao umefanyika katika kiwango cha kuridhisha.

 

Habari Zifananazo

Back to top button