Banana Zorro kufunga Bongo Fleva Honors leo usiku

DAR ES SALAAM; MSIMU wa kwanza wa onyesho la wasanii wakongwe linalofahamika kama Bongo Fleva Honors linahitimishwa usiku wa leo na mwanamuziki, Banana Zorro kwa shoo kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha watu wa Ufaransa (Alliance Francaise) Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Jukwaa hilo rapa mkongwe, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema Banana Zorro ndiye anafunga msimu wa kwanza ambapo wasanii nane hadi leo wameshapanda jukwaa hilo wakiwemo Dully Sykes, Tid, Juma Nature, Jaymoo, Mr. Bluu, Inspekta Haroon na Luten Karama kutoka kundi la Gangwe Mobb.

“Wasanii wakongwe watakaopata nafasi katika jukwaa la wakongwe lazima wawe na vigezo kadhaa ikiwemo kufanya shoo jukwaani kwa saa mbili bila kupumzika.

Sugu anasema msimu wa pili utaanza Januari 2024 na wasanii wote wakongwe wenye uwezo wa kuimba live watapata nafasi za kutumbuiza katika jukwaa hilo.

“Msimu wa pili utaanza Januari na tuna ratiba ndefu takribani miaka mitatu maana hadi leo wakongwe AY, Mwana FA, Fid Q bado hawajapanda na msimu ujao tutaendelea kuboresha kila mwaka nia ni kutunza historia ya muziki wa bongo fleva” amefafanua Sugu.

Pia Sugu ameeleza kwamba changamoto kubwa waliyokutana nayo kwa msimu wa kwanza ni kukosekana kwa wadhamini hivyo anaomba makampuni mbalimbali wadhamini jukwaa hilo ili wasanii wakongwe wainuliwe zaidi.

“Onyesho letu si la kibiashara linalenga zaidi asili ya muziki hivyo tunahitaji makampuni mengi yatusaidie ili tusi kwame katika harakati za kumnyanyua msanii mkongwe.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button