EPZA yazungumzia ujenzi zaidi viwanda Bagamoyo

PWANI: Kamati ya Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji imepokea taarifa ya upembuzi yakinifu pamoja na mpango kabambe wa mradi wa bagamoyo unao husu eneo maalum la kiuchumi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mamlaka ya EPZA leo Septemba 13, 2023 Mkoani Pwani na kuhudhuriwa na sekta mbali mbali.

Eneo hilo lilitolewa na serikali kupitia Sheria ya ukanda maalum wa Bagamoyo lina ukubwa wa hekta 9800, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais -mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema eneo hilo tayari limepimwa na lina jumla ya hekta 5473 huku wananchi wakilipwa fidia hekta 2422 na zimesalia hekta 3320.

Advertisement

Mbali hayo ameongeza kuwa kwa kutaka kupasua zaidi anga kiuchumi Serikali iliamua kuanzisha maeneo maalumu ya kiuchumi 2004 na kuongeza kuwa mradi huo ni Uwekezaji wa wenye thamani ya Sh trioni 11, ambapo viwanda zaidi ya 200 vinatarajiwa kujengwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa pwani Abubakari Kunenge amesema hakuna kikwazo chochote katika kufanikisha hilo kwani tayari Wananchi wamehusishwa katika mchakato huo na wapo tayari kupokea mradi huo.

Hatatahivyo mkurugenzi Mkuu wa EPZA Charles Itembe  amesema kupitia mradi huo Taifa litafaidika pakubwa katika Miradi ya Viwanda na kukuza uchumi wa nchi.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *