Bandari ya Mtwara kufungua zaidi mauzo ya Korosho

MTWARA: Bandari ya Mtwara inatarajia kupokea meli tisa zenye makasha matupu zaidi ya 2,758 kwa ajili ya kupakia korosho ghafi kwenda nje ya nchi.
Kaimu Meneja Bandari ya Mtwara, Duncan Kazibure amesema hayo leo tarehe 27 Novemba, 2023 katika kikao kazi cha kujadili mwenendo wa mauzo ya Korosho nchini.

Kazibure amesema makasha hayo yatakuwa na uwezo kupakia zaidi ya tani 105,000 za korosho ghafi.
Amesema hizo zitakazoleta makasha ni za makampuni ya CMA,CGM, PIL na MSC,
Kazibure amesema bandari mpaka sasa imepokea jumla ya makasha matupu 2,650 kutoka Kampuni mbalimbali yakiwemo makasha yenye uwezo wa kufungasha tani 100,954.4 za korosho.
“Kuna mahitaji ya wastani wa makasha matupu 3,779 yatakayoweza kupakia ,zaidi ya tani 143,968 ili kukamilisha zoezi zima la kusafirisha zaidi ya tani 350,000 hadi kufikia mwisho wa msimu,” amesema.

Amesema bandari hiyo imejipanga kushawishi kampuni za meli ili kufanikisha ongezeko la upatikanaji wa meli na makasha matupu kutimiza lengo la usafirishaji wa Korosho kupitia bandari hiyo.
 

Habari Zifananazo

Back to top button