Bandari ya Mtwara yazidi kufunguka

Bandari ya Mtwara.

MELI ya 13 imeingia katika Bandari ya Mtwara kupakia tani 22,000  za makaa ya mawe kuyapeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC).

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ahmed Abbas alisema anafarijika kuona Bandari ya Mtwara inazidi kufunguka.

Abbas alitoa rai kwa wasafirishaji wengine waendelee kutumia bandari hiyo kwa sababu kuna uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali hasa upanuzi wa bandari hiyo.

Advertisement

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jitegemee Holdings,  Emmanuela Kaganda alisema mwezi ujao watasafirisha  pia tani 40,000 za makaa ya mawe kupeleka nchi za Falme za Kiarabu.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara,  Norbert Kalembwe alisema meli hiyo ya 13, ilifika na kuanza kupakia juzi .

Mkurugenzi wa Wakala wa Kampuni ya Meli ya Express Chartering Shippingi Ltd Nchini (ESL), Esther Mbuya alisema kuwa wameanza kwa kasi ya hali ya juu .