KIUNGO wa Yanga, Yannick Bangala amesema hawapaswi kuwadharau wapinzani wao waliopangwa nao kwenye hatua ya Robo Fanaili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,, kwa sababu hatua waliyofikia inathibitisha ubora wao.
Akizungumza na HabariLEO, mchezaji huyo amesema kitu cha msingi kwao ni kutumia muda uliopo kujipanga na kurekebisha mapungufu yao, ambayo yalijitokeza kwenye mechi za hatua ya makundi ili waweze kutimiza malengo yao.
“Nikweli Yanga tuna kikosi bora, lakini huwezi kuwabeza Rivers United ni timu bora na ndio maana imefika hatua hiyo, kitu cha msingi ni kuwaheshimu na kuweka nguvu kwenye maandalizi yetu kabla ya kukutana nao nadhani tutafanikiwa lakini kama tutawadharau wanaweza kututoa tukabaki na majuto,” amesema Bangala.
Timu hizo zilishawahi kukutana kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita na Yanga kufungwa mechi zote mbili na kutupwa nje ya michuano hiyo.