TETESI zinaeleza Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo Yannick Bangala kutoka Young Africans.
Imeelezwa uhamisho huo ni baada ya Yanga kutomjumuisha kwenye kikosi kilichotajwa kwa ajili ya msimu ujao hata hivyo taarifa zinaeleza Bangala aliomba kuondoka Yanga siku kadhaa zilizopita.
Azam huenda ikamtambulisha Bangala muda wowote kuanzia sasa.
Usajili huo utakuwa wa pili kwa wachezaji kutoka Young Africans, baada ya miezi miwili iliyopita kukamilisha usajili wa Feisal Salum.
Comments are closed.