Bangi zamponza, ahukumiwa miaka 20

kilio kimbilio lake

MWANZA: Mkazi wa Kisiwa cha Maisome Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, Maisala Ramadhani (25) ameangua kilio mahakamani baada ya kuhukumiwa jela miaka 20 kwa kukiri kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi nyumbani kwake.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 121/2023, imetolewa Novemba mosi, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka.

Awali akisoma maelezo mbele ya hakimu, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Morice Mtoi alisema mshitakiwa alikamatwa Oktoba 9, 2023, na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Titho Mohe.

Mwendesha mashtaka huyo alisema mshtakiwa alikamatwa na askari huyo katika kisiwa cha Maisome kambi ya wavuvi ya Migongo akiwa na bangi kilogramu 10 kwenye nyumba yake ya kuishi.

Pamoja na maombi ya mshtakiwa (Maisala) kuomba kupunguziwa adhabu, Mahakama imemhukumu kifungo hicho cha miaka 20 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo kulingana na madhara yasababishwayo na madawa ya kulevya.

Habari Zifananazo

Back to top button