Bao la Man City lamuibua Wenger

KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anashangazwa kwa nini waamuzi hawakujiridhisha zaidi na goli lilofungwa na Machester City kwenye mchezo wa nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Goli lilofungwa na Kelvin De Bruyne lilionekana kuwa na dosari, ambapo kabla ya goli hilo mpira ulionekana kuwa nje ya eneo la kuchezea, hali iliyosababisha kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kulimwa kadi ya njano kwa kuzozana na waamuzi wa mchezo huo na Wenger anasema tukio hilo lilipaswa kufuatiliwa zaidi, ili kuondoa utata.

” Kwenye tukio kama lile walipaswa kulifuatilia na hawakwenda¬†mbali zaidi, ili kujiridhisha kama mpira ulikuwa ndani ya eneo la kuchezea ama nje.

“Ninafikiri walipaswa kutumia njia mbadala kwa sababu kikawaida VAR haitizami mistari ya pembeni, bali inajikita zaidi¬† eneo la mstari wa kwenye goli,” amesema.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelott yeye alilia na waamuzi wa mchezo huo akiamini hawakuitendea haki timu yake.

“Mpira ulikuwa nje teknolojia imeonesha hivyo, sjui kwa nini VAR haikulitizama hilo, mwamuzi hakuwa makini kwenye matukio mengi uwanjani, ” amesema.

Baada ya matokeo hayo ya sare bado mchezo huo unaonekana kuwa wazi kwa timu zote mbili kuelekea mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa kwenye dimba la Etihad.

Habari Zifananazo

Back to top button