Barabara Km 31 kujengwa Mbagala

DODOMA; Serikali imesema kupitia Mradi wa DMDP zimependekezwa kujengwa kilomita 31.82 kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Zainab Katimba amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo, aliyehoji ni barabara zipi zimetengewa fedha katika mradi wa DMDP awamu ya kwanza na barabara zipi zipo DMDP awamu ya pili katika jimbo la Mbagala.

“Kupitia mradi wa DMDP awamu ya pili zimependekezwa kujengwa kilomita 31.82 kwa kiwango cha lami katika barabara za; Ndunguru, Masaki, Masuliza, Maandazi, Kipati, Agape, Kilimahewa, Chasimba, Chamazi Magengeni, Saku na Tambani.

“Hadi sasa tayari barabara za urefu wa kilomita 18.48 zimesanifiwa na hatua za manunuzi zinaendelea,” amesema Naibu Waziri.

Amesema awamu ya kwanza ya mradi huo wa DMDP zimejengwa barabara katika kata tatu za Kijichi, Mbagala na Mbagala Kuu.

Habari Zifananazo

Back to top button