BUNGE la Bajeti linatarajiwa kuendelea leo na wizara tatu zinatarajiwa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Ratiba iliyotolewa na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi inaonesha kwamba leo Wiazra ya Ujenzi na Uchukuzi itawasilisha baejti na itajadiliwa kwa siku mbili.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) itafuatia na bajehi hiyo itajadiliwa kwa siku moja ikifuatiwa na bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itakayojadili kwa siku mbili.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa anatarajiwa kuwaeleza wabunge mafanikio na changamoto katika masuala ya ujenzi na uchukuzi sanjari na vipaumbele na mikakati katika mwaka wa fedha 2023/24.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa anatarajiwa kulieleza bunge masuala ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi sanjari mafanikio yaliyopatikana katika utekeleezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula anatarajiwa kuwaeleza wabunge mafanikio katika utekekezaji wa baeti ya sasa, changamoto, mikakati na miradi yenye lengo la kuboresha suala la upangaji wa miji na kupunguza changamoto za ardhi kwa wananchi.