Barabara ya Masumbwe, Ushetu yaanza kuboreshwa

WAKALA ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Shinyanga imeanza zoezi la kuboresha barabara kutoka Masumbwe mkoani Geita kuelekea Halmashauri ya Ushetu Mwambomba hadi Ulowa mkoani Shinyanga.

Hayo yamesemwa Leo na meneja wa Tanroads mkoa Mhandisi Mibara Ndirimbi akiwa ameambatana na mbunge wa Jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani huku akieleza kipande hicho Cha Barabara kina urefu wa kilomita 65.87.

Meneja alisema Barabara hiyo imepandishwa hadhi kuwa ya Tanroads tangu mwaka 2021/2022 kutoka chini ya usimamizi wakala wa barabara mjini na vijijini (Tarura).

” Barabara zilizo pandishwa hadhi mkoani Shinyanga ni urefu wakilomita 171.26 kwa mwaka 2023/2024 ambazo zitapangiwa fedha “alisema Mhandisi Ndirimbi.

Mbunge Cherehani amesema Sasa barabara zote zimeanza kupitika zinaunganisha Mikoa ya Geita na Tabora zinawanufaisha wafanyabiashara kusafirisha mazao yao vizuri wakati wa mavuno.

Habari Zifananazo

Back to top button