Barabara ya Nyerere -Shaurimoyo kufungwa miezi 3

BARABARA ya makutano ya Nyerere na Shaurimoyo itafungwa kesho kwa ajili ya ujenzi wa daraja la reli  ya Kisasa ya SGR.

Taarifa ya Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam inasema kuwa barabara hiyo itafungwa kuanzia kesho Mei 28 hadi Septemba 30, 2023 baada ya ujenzi husika kukamilika.

Taarifa hiyo imesema katika kipindi hicho cha ujenzi, vyombo vyote vya moto pamoja na watembea kwa miguu wanashauriwa kutumia barabara ya Kawawa, Veta- Chang’ombe, Shaurimoyo, Kilwa Road na barabara ya mchepuko iliyojengwa pembezoni mwa eneo hilo la ujenzi.

Advertisement