Baraza la Wazee Mtwara lampongeza Rais Samia

BARAZA Maalum la Wazee wa Kimila Wilaya ya Mtwara mkoani humo limetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliyotukuka wa kuwaletea watanzania maendeleo ukiwemo wa mkoa wa Mtwara.

Akizungumza mkoani mtwara katika kikao cha uzinduzi rasmi wa baraza hilo, Katibu wa Baraza hilo Selemani Nahatula amesema Rais huyo  katika uongozi wake huo amekuwa akitekeleza miradi ya maendeleo kwa watanzia kupitia sekta mbalimbali.

Baraza hilo limeundwa kwa lengo la kutaka kuwa karibu na viongozi, wananchi ili kuhakikisha kazi na maendeleo ya wilaya hiyo zinaenda vizuri, kurekebisha tabia na mienendo ya watu kwa kuhakikisha viongozi waliyopo madarakani wanasimamia vizuri utekelezaji wa majukumu yao.

Miradi  hiyo inayotekelezwa kupitia serikali ya awamu ya sita chini ya Rais huyo na uongozi wake wote kwa ujumla ngazi za kitaifa na za chini ikiwemo sekta ya elimu, afya, maji na mingine lakini kubwa zaidi wananchi wa mkoa huo walikuwa na kiu kubwa kuona bandari ya mtwara inatumika kikamilifu hasa usafirishaji wa zao la korosho.

‘’Kwasababu zao kuu la biashara mkoa wa Mtwara ni korosho  na korosho zikisafirishwa kupitia bandari ya mtwara maana yake ni kufungua fursa ya ajira kwa vijana ikwemo wachukuzi wanaoshusha na kupakia magunia bandarini, wanawake,  mama lishe’’amesema Nahatula

‘’Popote pale kwenye maghala hapa mjini kila kona utakayopita utagundua kuwa wananchi hasa akina mama wanawahulisha korosho kuweka kwenye magunia na kushonea tayari kwa kupelekea bandarini ili ziweze kusafirishwa kupelekwa nchi za nje’’

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Selemani Liloko ‘’Baraza hili la wazee lilikuwepo tangu miaka mingi, tangu enzi hizo ila tulikuwa bado hatujajitambulisha sasa leo tumeamua kujidhihilisha rasmi hapa uwanjani kwa kuwapongeza viongozi wetu’’amesema

Mjumbe wa Baraza hilo, Asha Mbani amesema wazee hao  sehemu kubwa wamekuwa wakitumika katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa ujumla wilayani humo ikiwemo ushauri  na kusimamia yale mazuri lakini pia kukanusha upotoshaji.

Habari Zifananazo

Back to top button