BARCELONA,Hispania: RAIS wa Barcelona Joan Laporta amesema wamepokea dau la euro milioni 200 kwa ajili ya kumuuza mchezaji wao Lamine Yamal (27) kipindi hiki cha majira ya joto lakini rais huyo amekataa ofa hiyo.
Laporta amesema pia Barcelona haitawauza wachezaji wake wengine sita wanaotakiwa na timu mbalimbali akiwemo Alejandro Balde (21), Fermín López (21), Pedro González (22), Frenkie de Jong (26), Ronald Federico (25), Pablo Martín (19).
“Tunapokea zabuni za kijinga kwa wachezaji wetu sita akiwemo Lamine Yamal kwa euro milioni 200 tumekataa, bila shaka hatuuzi wachezaji wetu wote sita,” amesema Laporta.
“Tunamwamini Lamine na tunahitaji huduma yake hivyo hatumuuzi. “Tumepokea dili lingine kwa ajili ya wachezaji wetu wengine sita akiwemo Alejandro Balde (21), Fermín López (21), Pedro González (22), Frenkie de Jong (26), Ronald Federico (25), Pablo Martín (19) nalo tumekataa hatutaki kuwauza nyota wetu.” Ameeleza Laporta.
Laporta amesisitiza kwamba wataendelea kuongeza wachezaji ili kuijenga Barcelona kabla ya msimu ujao na si kuwauza nyota wao.