Bares aichimba mkwara Ihefu
SINGIDA: Kocha mkuu Klabu ya Mashujaa, Abdallah Mohammed maarufu Bares amesema mchezo wao robo fainali ya kombe la shirikisho la CRDB dhidi ya Ihefu ya utakuwa mgumu lakini Ihefu wanapaswa kuwaheshimu.
Bares ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo uliofanyika mjini Singida.
“Utakuwa ni mchezo mgumu lakini tumejipanga kikamilifu kukabiliana na mchezo wa kesho, tunawaheshimu Ihefu hivyo na wao wanatakiwa kutuheshimu.” – Amesema kocha huyo.
Kwa upande wake mchezaji wa kikosi hicho Adam Adam amesema wao kama wachezaji wamejiandaa kuikabili Ihefu na wako tayari kutekeleza maelekezo ya kocha ili wapate ushindi utakaowapeleka nusu fainali ya kombe hilo.
“Tumejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo wa kesho, mwalimu kafanya kazi yake kwenye uwanja wa mazoezi kazi imebaki kwetu wachezaji kuyafanyia kazi maelekezo ya mwalimu wetu.” – Amesema Adam Adam.
Mashujaa watakuwa wageni wa wajukuu waa mbogo maji Ihefu katika dimba la CCM Liti mjini Singida kuanzia saa 10:00 jioni Jumatano Mei mosi 2024.