Basata yatoa neno ‘video’ watoto wakiimba

BARAZA la Sanaa Taifa ( BASATA) halijafurahishwa na kitendo cha watoto kuonekana kwenye ‘video’ ikionesha watato ambao wamesema wanakadiriwa kuwa na umri usiozidi miaka 10 wakiimba wimbo wenye maudhui yasiyokuwa na maadili kwa makuzi ya mtoto.

Katika taarifa yao iliyotolewa leo Machi 4, 2023 na kitengo cha mawasiliano cha baraza hilo, imeeleza kuwa wanaamini kitendo hicho kimefanywa na mtu mzima mwenye nia ovu ya kuharibu maadili mema ya ustawi wa mtoto.

“Basata inatoa rai kwa Wananchi wote kutumia kazi mbalimbali za sanaa kuelimisha jamii na siyo kupotosha, pia wananchi wasiendelee kusambaza video hiyo ili kuondoa madhara yanayoweza kuwakumba watoto hao”. Imeeleza taarifa hiyo.

Advertisement

Hivi karibuni kumekuwa na ‘video’ fupi inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha watoto ambao wakiimba wimbo usiokuwa na maadili.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *