Bashe aahidi neema kwa wakulima nchini

DAR ES SALAAM: SERIKALI ya Tanzania imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya kilimo kutumia teknolojia za kisasa ili kukuza biashara ya kilimo nchini.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye Mkutano na wawekezaji wa ndani katika sekta ya kilimo leo, jijini Dar es salaam.

Advertisement

Amesema bajeti ya taifa katika sekta ya kilimo imekuwa ikiongezeka kila uchwao, kutoka Dola za Kimarekani milioni 125. 06 mwaka 2021/2022 hadi Dola 322.9 mwaka 2022/2023 na kufikia Dola 413.9 milioni mwaka 2023/2024 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 28%.

 

Bashe amesema wizara inatakiwa kuendelea kujenga sekta ya kilimo endelevu na shindani ili kukuza uchumi shirikishi kwajili ya kuboresha maisha ya wakulima na kupata matajiri ili kufikia ukuaji wa kijani.

Aidha alieleza kuwa wizara imeweka mikakati ya kuboresha ukuaji wa uchumi wa wawekezaji wa ndani katika kilimo sambamba na  kuwapa wakulima ardhi kwa makubaliano ya utendaji kazi ambayo yatasimama kama malipo badala ya malipo ya fedha taslimu.

 

 

Kwa upande wake Waziri wa Mipango na Uwekezaji Kitila Mkumbo amesema ipo haja ya kupunguza kanuni zinazowapa wawekezaji wakati mgumu katika kulipa kodi na kuleta uhuru wa kiuchumi ili kuondokana na umaskini.

Kitila amewataka wawekezaji kuongeza mauzo ya nje ya nchi vifaa vya kilimo vilivyoongezwa thamani (bidhaa za viwandani) itarahisisha kuleta maendeleo na kuendelea kuongeza Pato la Taifa (GDP) la Taifa.

 

Kwa upande wake Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amesema Tanzania sasa inaendelea kujiondoa kwenye mnyororo wa umaskini ikiwa ni mkakati wa kuondoa umasikini.

 

Pia amejitolea kuongeza bajeti kwa wizara ili kufikia lengo la kuimarisha sekta ya kilimo, na kuchukua hatua zaidi kwa kuongeza uzalishaji zaidi na kuuza nje zaidi ambayo itaongeza fedha za kigeni.

 

Katika hatua nyingine viongozi hao waliweza kuzindua nembo mpya ya Mamlaka  ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *