Bashungwa ambana mkandarasi, atoa siku 14

MBEYA: Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa siku 14 kwa Wakala wa Barabara (TANROADS), Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga barabara ya Ibanda – Kajunjumele – Kiwira/Itungi Port (km 32) analeta vifaa na watalaam wote wanaohitajika eneo la mradi kwa mujibu wa mkataba.
Mradi wa barabara hiyo unafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100 kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 38 ambapo unatekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya M/s AVM-Dillingham Construction International na kusimamiwa na Kitengo cha TECU kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS).
Bashungwa ametoa agizo hilo Oktoba 2, 2023 wilayani Kyela mkoani Mbeya mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo ipo nyuma ya muda wa mkataba kwa asilimia 25 na kubaini mradi huo una upungufu wa watalaam na vifaa muhimu vinavyohitajika eneo la mradi.
“Naiagiza TANROADS, CRB na ERB kunipa taarifa ndani ya siku hizo na kama mkandarasi akishindwa kutekeleza kama mkataba unavyosema na tutalazimika kuchukua hatua ngumu basi tuzichukue haraka iwezekanavyo”, amesema Bashungwa.
 
Bashungwa ameeleza kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekwishatoa fedha kiasi cha Bilioni 3.7 kama sehemu ya malipo ya kwanza ya awali ya ujenzi huo na hadi sasa mkandarasi amekwishafanya maandalizi kwa asilimia 15 tu ukilinganisha na mahitaji ya mkataba.
“Kama unataka kujua rangi ya Rais chezea hii hela aliyoitoa Dk.Samia… Mkandarasi umepewa hela ndo unaenda kufanya manunuzi ya vifaa Uturuki wakati ulitakiwa uwe navyo tayari na kuvileta eneo la mradi kipindi cha maandalizi”, amesisitiza Bashungwa.
Bashungwa ameeleza kuwa anafahamu mkandarasi huyo amepewa tena ujenzi wa barabara ya Sengerema – Nyehunge (km 54.4) ambapo ametilia shaka kasi ya mkandarasi huyo ambayo anaenda nayo  kama ataweza kutekeleza mradi huo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
KelleighIdelle
KelleighIdelle
2 months ago

Google paid 99 dollars an hour on the internet. ( 44q) Everything I did was basic Οnline work from comfort at home for 5-7 hours per day that I got from this office I found over the web and they paid me 100 dollars each hour. For more details
visit this article————>> http://Www.SmartCareer1.com

Dona
Dona
Reply to  KelleighIdelle
2 months ago

I g­e­t­ o­v­e­r­ ­­2­5­k­ ­u­s­d­ ­a­ ­m­o­n­t­h­ ­w­o­r­k­i­n­g­ ­p­a­r­t­ ­t­i­m­e­.­ ­I­ ­k­e­p­t­ ­h­e­a­r­i­n­g­ ­o­t­h­e­r­ ­p­e­­o­p­l­e­ ­t­e­l­l­ ­m­e­ ­h­o­w­ ­m­u­c­h­ ­m­o­n­e­y­ ­t­h­e­y ­c­a­n­ ­m­a­k­e­ ­o­n­l­i­n­e­ ­s­o­ ­I­ ­d­e­c­i­d­e­d­ t­o l­o­o­­k ­i­n­t­o­ i­t. W­e­l­l­,­ ­i­t­ w­a­s­ ­a­l­l­ ­t­r­u­e ­a­nd h­a­s to­t­a­l­ly ch­a­n­g­e­d­ ­m­y l­i­f­e­…T­h­i­s i­s w­h­a­t I­ d­o,C­o­p­y B­e­l­l­o­w ­W­e­b­s­i­t­e

Just open the link———————->> http://Www.Smartcash1.com

Last edited 2 months ago by Dona
MAPESA1234567
MAPESA1234567
2 months ago

HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE

money
money
2 months ago

ULIMWENGU WA NDOTO

One.  DEREVA BODABODA ANA NDOTO YA KUMILIKI KAMPUNI YA NDEGE

Two.    MUUZA MBOGAMBOGA ANA NDOTO YA KUMILIKI KIWANDA CHA MBOGA MBOGA

Three.             MUUZA VITUNGUU SUMU ANA NDOTO YA KUMILIKI KIWANDA CHA VITUNGUU SUMU 

Four.  MUUZA NYANYA ANA NDOTO YA KUMILIKI KIWANDA CHA NYANYA

Five.    MUUZA MAJI ANA NDOTO YA KUMILIKI KIWANDA CHA NDEGE

Six.         MUUZA BAR ANA NDOTO YA KUMILIKI KUJENGA BAR

Seven.          MUUZA FREMU ANA NDOTO YA KUMILIKI SHOPPING MALLS

Eight. MGANGA WA KIENYEJI ANA NDOTO YA KUMILIKI HOSPITALI

Nine. MPIGA DEBE ANA NDOTO ZA KUMILIKI KAMPUNI YA MABASI

Upo sahihi “tukasomeeeeeee tueleweeeeeee Saaaana

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x