Bashungwa amsimamisha kazi DED Muheza

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza mkoani Tanga, Nassib Bakari Mmbaga kuanzia leo Agosti 30 kupisha uchunguzi.

Taarifa ya TAMISEMI imesema Bashungwa amechukua uamuzi huo baada ya Mmbanga kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Pia ametaka Wakurugenzi wote kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma. 

Advertisement
1 comments

Comments are closed.

/* */