Bashungwa asifu utendaji wa Rais Samia

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi madhubuti mwenye maono ya kufikili na kuona mbali kwa ajili ya Watanzania.

Bashungwa alieleza hayo katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo.

“Rais nakupongeza kwa dhati ya moyo wangu kwa uongozi wako madhubuti, hakika umekuwa faraja kwa Watanzania wote. Wewe ni Rais mwenye maono ya kuona mbali.” Amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema Rais Samia Katika uongozi wake madhubuti yapo mamaamuzi ya kijasiri amefanya na ataendelea kuyafanya na wapo watu watamkatisha tamaa lakini asikate tamaa Watanzania watakumshukuru baadaye.

“Yapo maamuzi magumu ya kijasiri unayafanya Rais lawama zitakuwepo leo lakini Watanzania tutakushuru baadaye” amesema Bashungwa.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button