WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amelielekeza Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kuongeza eneo la kilimo cha mpunga katika kikosi cha uzalishaji mali cha Chita JKT kilichopo mkoani Morogoro.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake katika kikosi hicho ambacho ni miongoni mwa vikosi vya uzalishajimali vya JKT.
Alisema pamoja na kazi kubwa ya kulima mpunga kwa ajili ya chakula na mbegu ekari 3,500 za sasa ni vyema kila mwaka wakaongeza ukubwa wa eneo na hatimaye kufikia ekari 12,000.
Jeshi la Kujenga Taifa ni taasisi kubwa na hapa zipo ekari 12,000 zinapaswa kuendelezwa, hivyo tukitoka hapa tunakwenda kujipanga kuhakikisha uzalishaji huu wa mbegu na kilimo mkakati unaongezeka kila mwaka ili ekari zote 12,000 tuweze kuzitumia kimkakati kusaidia kwenye suala zima la usalama wa chakula na kusaidia vijana wanaojiunga na JKT kupata ujuzi na stadi za kazi zaidi.” Amesma
Kuhusu ufugaji wa samaki, Bashungwa ameipongeza JKT kwa ubunifu huo ambao unajumuisha kilimo cha umwagiliaji na ufugaji kwa pamoja.
“ Miradi mbalimbali kilimo na ufugaji inayotekelezwa na JKT ni jitihada na ubunifu wa JKT kuangalia namna ya kusaidia juhudi za serikali za kuzalisha ajira kupitia mafunzo stadi wanayopewa vijana wa JKT, kupitia miradi hii vijana wanaomaliza mafunzo wanakuwa na stadi za kuweza kujiajiri na kuajirika.”Amesema
Naye Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Rajabu Mabere alisema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mwaka 2021/2022 ilitenga Sh 4 bilioni kwa JKT za kununua mitambo.
“Hata katika bajeti hii inayoendelea ya mwaka 2022/2023 vile vile imeona umuhimu wa kutuwekea kiasi fulani (cha fedha) ili tuweze kununulia mitambo na kuboresha miundombinu ambayo inaweza kuchukua vijana wengi zaidi kuingia katika Jeshi la Kujenga Taifa,”alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha 837, Luteni Kanali Emmanuel Kukula amesema katika utekelezaji wa kilimo mkakati wameanza na ekari 2,500 ambayo ikimalizika inatarajiwa kutumia Sh bilioni 8.6