Bashungwa ziarani Iringa
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Iringa, Halima Dendego, leo tarehe 05 Oktoba 2023.
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atashuhudia utiaji saini wa ujenzi wa barabara ya Ipogolo hadi Kilolo yenye km 33.
6 kwa kiwango cha lami na kukagua ujenzi uwanja wa ndege wa Mkoa wa Iringa.
Aidha, Waziri Bashungwa atakagua barabara ya mchepuo ya Iringa (Eneo la Igumbilo stand na njia panda ya Chuo Kikuu cha Iringa) pamoja na eneo la barabara katika Mlima Kitonga.