ABIRIA 57 waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Al- Sayyed lenye namba za usajili T 995 DLB kutoka Wilaya ya Kilosa kwenda jijini Dar es Salaam, wamenusurika kufa, baada ya basi hilo kupinduka eneo la Kitungwa, Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Morogoro, Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Desemba 28, 2022 majira ya asubuhi barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
Amesema kondakta wa basi hilo Seif Omary Mwandagilo (30), mkazi wa Gairo, amelazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi, wakati abiria wote waliopata majereha madogo walipatiwa huduma ya kwanza eneo la tukio na kuendelea na safari, baada ya kutafutiwa basi lingine.

Kamanda amesema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, waliwasili haraka na kutoa msaada wa kibinadamu ikiwemo huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi la Kampuni ya Ally’s Star lenye namba T.
947 AND likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza, kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Kamanda Musilimu amesema dereva wa basi la Al-Sayyed katika kukwepa, ili kuepusha ajali ya kugongana uso kwa uso, ilimlazimu kutoka nje ya barabara, ndipo basi lake liliposerereka na kupinduka.
Amesema dereva wa basi la Ally’s Star, alishikiliwa na Polisi baada ya kuingia Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu.
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me.