Basi la mwendokasi lililokuwa linatokea Kivukoni laparamia duka eneo la Kisutu, Ilala, Dar es Salaam asubuhi hii, watu kadhaa wajeruhiwa.
Taarifa za awali zinaonesha kuwa kuwa dereva wa basi la mwendokasi alikuwa anajaribu kulikwepa gari dogo aina ya Noah lililokuwa likikatiza barabara ya BRT bila tahadhari.
“Kuna watu nimeona wamejeruhiwa wakiwemo wanafunzi,” mpita njia amelieleza HabariLeo.
Hata hivyo timu ya waandishi wa TSN Digital imefika eneo la tukio.
Taarifa zaidi kukujia.