Basi latumbukia Mto Pangani

Basi la kampuni ya Moa linalifanya safari zake kati ya Tanga na Pangani na kuvuka kwa kivuko kwenda Kipumbwi, limetumbukia kwenye Mto Pangani wakati linatoka kwenye kivuko cha Mv Tanga.

Tukio hilo limetokea eneo la Feri ya Bweni majira ya Saa sita mchan leo Jumapili Julai 23, 2023,  ambapo wakati linatoka katika kivuko  kuendelea na safari lilipata  hitilafu kwenye mifumo ya breki.

Akizungumza  kwenye eneo la tukio, Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah, amesema kuwa hakuna madhara ya mali wala binadamu katika tukio hilo .

Advertisement

“Basi lilizama wakati linataka kutoka katika kivuko baada ya kufika feri ya Bweni, ndio likashindwa kupanda, hivyo likatumbukia kwenye maji, lakini tumefanikiwa kulitoa na huduma za kivuko sasa zinaendelea kama kawaida,” amesema.

 

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *