Bavicha: Uzoefu wa kazi usiwe kigezo cha ajira

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), John Pambalu ameiomba serikali kulegeza kigezo cha uzoefu wa kazi kama mojawapo ya sharti la ajira kwa vijana.

Pambalu alisema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

“Ipo haja serikali kulegeza masharti ya ajira kwa vijana kwa kuwa kwa sasa vijana wengi wanakosa ajira kwa kigezo cha uzoefu wa kazi na badala yake wapewe kazi chini ya usimamizi wa kipindi cha miezi kadhaa au miaka kadhaa,” alisema.

Pambalu alisema ipo haja uchunguzi ufanyike kwa kina kuhusu walengwa na wanaopata mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri kwa vijana kwa kile alichodai kuwa mikopo hiyo hutolewa kwa upendeleo.

Aliiomba serikali itoe masharti nafuu kupitia taasisi za kifedha hususani zile za serikali ili kijana anapohitimu masomo ajiajiri na kufanya biashara.

Akijibu maswali ya waandishi kuhusu kufanya siasa za kistaarabu na si za matusi alisema swali hilo viulizwe vyama ambavyo havina sera na ilani.

“Sisi ni chama chenye Sera, Ilani na Katiba hivyo kusema tutafanya siasa za matusi siyo sahihi, kwenye mikutano yetu tutafanya mikutano kwa kutoa hoja za kitafiti na siyo matusi na kazi yetu ni kuielekeza serikali,” alisema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x