Bawacha wampa 5 Rais Samia kuboresha Demokrasia
BARAZA la Wanawake la Chadema (BAWACHA) limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha Demokrasia nchini.
Akizungumza leo Machi 8, 2023, Mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu amesema mwenendo mwema wa Rais Samia unafifisha kila siku hofu iliyokuwa imewatanda.
“Nimesimama hapa bila kuwa na hofu ya kukamatwa na Polisi wala kurushiwa mabomu, mama pokea baraka nyingi za Mungu.”Amesema Grace na kuongeza
“Mwenendo wako mwema, umeboresha demokrasia na haki nchini, hatua na mwenendo wako mwema kila dalili zinaendelea kufifia kila siku, maisha yetu ya awali katika serikali ya mtangulizi wako yalijaa hofu, kuwasiliana ilikuwa shida, kutengamana, kutekwa, kunyanyaswa , kuteswa na vilio.
“ Wewe ni Mwenyekiti pamoja na Mwenyekiti wetu Mbowe (Freeman) mmeibuka katika jahazi la siasa na kubaidli mwelekeo, vilio vya kupokwa ushindi katika uchaguzi mmebadilisha.”Amesema na kuongeza
“Karibu Mkoa wa wajanja, zamani mkoa huu ulikuwa ni kati ya mikoa ya baridi, lakini sasa hivi ni joto kutokana na uharibifu wa mazingira.” Amesema Kiwelu
Kiwelu, amewashtaki baadhi ya watendaji wa serikali walioweka vigingi ili wasipande miti na kudai kuwa wamezoea uhafidhina katika utawala uliopita ambao Maisha yalikuwa ni ya kunyanyasana na kubaguana na kusahau kuwa mfumo umebadilika.
“Mama kama tulivyokueleza kuwa Kilimanjaro imekuwa na joto kutokana na uharibifu wa mazingira, tulipanda Miti Kindi Dc zoezi hili lilitanguliwa na upinzani mkali kutoka kwa Mkurugenzi lakini badae tulipata upinzani na unyanyasaji mkubwa katika shule ya sekondari kiborloni….; “Ulivuka mipaka tulinyimwa kuotesha mmoja kati ya watumishi alifika na kututamkia haturuhusiwi kuotesha miti maana sio chama tawala, analinda ugali wake.”Amesema
|Aidha, Kiwelu amemshukuru Mwenyekiti wao Mbowe kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake bila kuyumbishwa licha ya misukosuko mingi aliyopitia.
“Mbowe amekuwa imara, hakuyumbishwi, licha ya mawimbi makubwa yaliyokuwepo lakini alivuka salama na leo tupo hapa kuwapa heko wanawake kutekeleza majukumu yao, kutekeleza majukumu yao katika ajira, kutekeleza majukumu yao majumbani na katika taifa kwa ujumla.”Amesema