ENDAPO Arsenal itachelewa kuwasilisha ofa yao kwa West Ham, huenda ikala kwao, imeripotiwa Bayern Munchen wameandaa pauni milioni 95 kumnasa kiungo Declane Rice.
Arsenal inataka kuimarisha eneo la kiungo ambapo Granit Xhaka imethibishwa kuwa atajiunga na Bayer Leverkusen.
Daily Mail wameripoti kuwa Arsenal imepeleka pauni milioni 90 kumnasa Rice ambaye pia kwa mujibu wa mtandao huo anawindwa na Man United.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema amedhamiria kufanya maboresho kwenye baadhi ya maeneo, lakini pia lazima baadhi ya wachezaji wauzwe kukamilisha hilo.