BAYERN Munchen na PSG zimekuwa timu za kwanza kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya ushindi wao wa mechi za usiku wa leo.
Bayern ilishinda bao 3-0 dhidi ya Lazio na hivyo kupindua matokeo ya 1-0 ya wiki mbili zilizopita. PSG ikiwa Reale Arena iliipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Sociedad na hivyo kwenda robo kwa ushindi wa mabao 4-1, baada ya ushindi wa 2-0 wiki mbili nyuma.
Mshambuliaji wa Bayern Munchen, Harry Kane alifunga mabao mawili, katika ushindi huo, Thomas Muller aliweka kambani bao moja.
Kwa upande wa PSG, Kylian Mbappe alifunga mabao mawili.