Bayern yamsimamisha Mane

BAYERN Munchen imemuadhibu kwa kumsimamisha mchezo mmoja pamoja na kulipa faini mshambuliaji wao Sadio Mane baada ya kumpiga sehemu ya mdomo mshambuliaji wa timu hiyo Leroy Sane.

Mane alifanya tukio hilo juzi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City, imeelezwa wachezaji hao walianza kujibizana kwa hasira, licha ya kugombelezewa na wachezaji wenzao.

Bayern atacheza na Hoffenheim katika mchezo wa Bundasliga wikiendi hii, Mane atakosa mchezo huo.

Licha ya adhabu hiyo Mane pia ameomba msamaha leo mbele ya wachezaji wenzake kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja.

Habari Zifananazo

Back to top button