WATANZANI wametakiwa kujenga utamaduni wa kujikatia bima ya maisha ili kuandaa kesho yao.
Hayo yamesemwa leo Juni 30, 2023 na Afisa Bima wa NIC Insurance, Zulfa Mngoya akizungumza na HabariLeo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Dar es Salaam
Amesema, NIC ina kifurishi cha bima ambayo inaitwa BeamLife inayomuwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo
“Bima ya Beam life ni bima ya uwekezaji ambayo umuwezesha mteja kujiwekezea kidogo kidogo kuanzia kiasi sh 5,000 na kuendelea kwa muda wa miaka mitano mpaka miaka 15.” Amesema Zulfa na kuongeza
“Katika bima hii tunampatia mteja faida ya uwekezaji pamoja na asilimia saba ya michango ya kila mwaka, mkataba ukifika mwisho tunampatia mteja kiasi alichochangia pamoja na zile asilimia saba ambazo zinajibeba mpaka mwisho wa mkataba.”Amesema
Amesema pia, wanatoa mkono wa pole ambao unaitwa ‘Funeral benefit’ ambayo ni asilima tano ya kile kima cha bima iwapo mwenye bima akifariki au kufiwa na wategemezi wake akiwemo mwenza wake au mtoto.
“Kwa sasa tupo sabasaba tumewasogezea huduma wateja wetu. Jiwekee bima kwa manufaa ya kesho yako kwa sababu beam life unaiandaa kesho yako kuanzia leo kutimiza malengo yako ya muda mrefu au mfupi.”Amesema Zulfa
Aidha, amesema katika bima hiyo hata ikitokea mwenye bima amepoteza maisha wategemezi wake watafaidika na ile pesa ambayo mwenye bima alichangia katika kipindi chote cha mkataba.
Comments are closed.