Bega Mwenyekiti mpya CCM Nyamagana

PETER Bega ameibuka kuwa Mwenyekiti mpya  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Wilaya ya Nyamagana, Yahya Lukonge, alimtangaza Bega kuwa mshindi, baada ya kupata kura 394 na wapinzani wake Zebedayo Athumai aliyepata kura 129 na Patrick Kambarage aliyepata kura 105 katika kura 628 zilizopigwa.

Lukonge ametangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, wakati wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa shule ya sekondari Nganza mkoani Mwanza.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Bega aliwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na wanachama wote.

Amewaomba wanachama wa CCM kuungana pamoja katika kuhakikisha wanakijenga chama chao, katika misingi ya amani na umoja.

Habari Zifananazo

Back to top button