Baleke, Sawadogo mtawaona kesho kwa Mkapa

Meneja wa Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mchezaji Jean Beleke atawasili kesho nchini na baada ya hapo ataelekea Uwanja wa Mkapa kusalimiana na mashabiki wa timu hiyo lakini hatocheza mchezo dhidi ya Mbeya City.

Beleke ni mshambuliaji aliyesajiliwa na timu hiyo akitokea Nejmeh ya Lebanon kwa mkopo, aliwahi kuitumikia TP Mazembe ya DR Congo.

Akizunguma hii leo mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally amesema ujio wa mchezaji hao utaambana na wa Sawadogo Ismaël ambaye atakuwepo kwa ajili ya kusalimia na mashabiki kuangalia mchezo huo.

“Kama atawasili mapema (Jean Beleke) naye ataelekea uwanjani kusamilia mashabiki, usajali huu unaenda kutibu matatizo tuliyokuwa nayo ni wachezaji mahususi kwa ajli ya maeneo yaliyolega.” amesema Ahmed.

Habari Zifananazo

Back to top button