MWANAMUZIKI Christian Bella, kundi la Twanga Pepeta na Msondo wanatarajia kufanya awamu ya pili ya tamasha la Grand Gala Dance mkoani Mbeya ili kuunga mkono sikukuu ya wakulima nane nane.
Akizungumzia juu ya tamasha hilo linaloandaliwa na Chocolate Princess ya Mboni Mashimba alisema hii ni mara ya pili kufanya tamasha hilo ambapo kwa mara ya kwanza lilifanyika Dr es Salaam mwaka janaja katika kuadhimisha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Alisema kutokana na mahitaji makubwa ya mashabiki, wamejikuta wakifanya mapema zaidi kwakuwa kusubiri siku kama hiyo ni kuwanyima haki ya burudani mashabiki zao.
“Ni tamasha ambalo litakuwa likiendelea kila mwaka, lakini kwa mwaka huu tumeona kitu kikubwa ndiyo maana tukaona tufanye mapema” alisema.
Alisema tayari tiketi za tamasha hilo zimeshaanza kuuzwa, hivyo ameomba mashabiki wa Mbeya na mikoa ya karibu kuweza kuwahi kununua kwakuwa zikiisha hawataongeza zingine.
Mwanamuziki Christian Bella alisema kwa muda mrefu alikuwa hajafanya tamasha katika mkoa huo, hivyo anaamini atafanya makubwa ikiwemo kuimba nyimbo zake pendwa na mpya.
Mboni alisema tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka ambapo Agost 7 mwaka huu litafanyika hapo katika ukumbi wa Tughembe Hall ikiwa na kauli mbiu ya kilimo na burudani.
“Wapenzi wa muziki wa dansi wote mnakaribishwa, hili ni tamasha Leno na litakuwa kubwa na tiketi zimeshaanza kuuzwa.” alisema