Ben Pol kutangaza Albamu Mikoa 15

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Bernard Paul, ‘Ben Pol’  amesema atafanya tour yake kuzunguka Mikoa 15 kutangaza albamu yake ya Flamingo yenye nyimbo 8 ambayo itazinduliwa  Oktoba 27  mwaka huu katika Hoteli ya Morena iliyoko jijini Dodoma.

Katika kutangaza albamu hiyo Ben pol amesema ataanza na Mkoa wa Dodoma ikiwa ndio Mkoa aliokulia na kulelewa akiwa na msanii mwenzake Darasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ben Pol amesema kuwa lengo ni kukutana na mashabiki kuweza kuongea nao na kuwapa burudani.

Advertisement

“Hii itakuwa albumu yangu ya tatu inayo kwenda kwa jina la Flamingo ambapo albumu hii inategemewa kuzinduliwa Tar 27 Oktoba 2023.

Aidha Ben amesema albumu hiyo imejawa na vibe kubwa na la kipekee ambapo imesimamiwa na msanii Darasa CMG.

Kwa upande wake Darasa amesema anaheshimu kipaji cha Ben, unajua uwezo mkubwa Ben alionao wa kuimba na kutumbuiza, na kuwa ni wasanii wachache sana Afrika Mashariki wenye uwezo na kipaji kama cha Ben Pol.

Ikumbukwe Ben Pol ni miongoni mwa wasanii wakongwe waliodumu kwenye chati kwa zaidi ya miaka 10 licha ya kubadilika kwa zama, na changamoto tofauti tofauti.

Hii ni sababu kubwa iliyomfanya achague jina la albamu yake kuwa “Flamingo”.

3 comments

Comments are closed.