Benchika kazi kwako sasa
MIONGONI* mwa silaha alizopewa kocha mpya wa Simba SC, Abdelhak Benchika ni kufanya kazi kwa uhuru bila kupangiwa maamuzi yoyote katika nafasi yake.
–
Ofisa Mtendaji Mkuu, Iman Kajula amesema Bodi ya Simba na Menejimenti imeamua kufanya hivyo kwa kuzingatia ukubwa wa timu hiyo Afrika.
–
“Sisi ni moja ya klabu bora Afrika hatuwezi kufanya kazi kwa kumbana.” Imani Kajula.
–
Kajula amesema kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili.