Benchikha aanza na ushindi

KOCHA mpya wa Simba SC, Abdelhak Benchikha ameanza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugra uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na Saido Ntibazonkiza, Sadio Kanouté na John Bocco.

Kocha huyo aliyesajiliwa wiki kadhaa zilizopita akitokea USM Alger, mchezo wake wa pili utakuwa dhidi ya Wydad Casablanca Ligi ya Mabingwa utakaopigwa Desemba 19, 2023.

Baada ya ushindi huo, Simba inaendelea kushika nafasi ya tatu, wakiwa na pointi 22, baada ya kucheza michezo tisa.

Vinara wa ligi ni Azam FC wenye pointi 28, wakiwa mbele kwa michezo mitatu dhidi ya Yanga na Simba wenye michezo idadi sawa.

Habari Zifananazo

Back to top button