DAR ES SALAAM: BAADA ya kuhudumu kwa takribani miezi mitano tu, leo uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, umethibitisha kuafikiana kuvunja mkataba na Kocha wao Mkuu, Abdelhak Benchikha sambamba na wasaidizi wake wawili.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo (CEO), Imaji Kajula inaeleza kuwa Mwalimu Benchikha ameomba kuvunja mkataba wake kutokana na matatizo ya kifamilia.
https://www.instagram.com/p/C6T_9-ds5hF/?utm_source=ig_web_copy_link
“Uongozi wa klabu ya Simba unamshukuru Mwalimu Abdelhak Benchikha kwa kipindi chote alichotumikia ndani ya timu yetu na tunamtakia kila la heri,” Simba imeeleza katika taarifa yake.
Katika hatua nyingine, klabu hiyo imemteua Mwalimu Juma Mgunda kukiongoza kikosi hicho akisaidiwa na Selemani Matola hadi hapo Bodi ya Wakurugeniz itakapotoa uamuzi mwingine.
“Mwalimu Mgunda ataanza kazi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC mnamo Aprili 30 mwaka huu katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi,” imeeleza taarifa hiyo.